IQNA

Maulidi

Mji mkuu wa Yemen  waandaliwa kwa ajili ya sherehe za Milad-un-Nabi

21:32 - September 09, 2024
Habari ID: 3479404
IQNA - Mamlaka na watu huko Sana'a, mji mkuu wa Yemen, katika wiki za hivi karibuni wamekuwa wakifanya maandalizi ya kufanya Sherehe za Milad-un-Nabi. Sherehe hizi ni za kila mwaka hufanyika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Sherehe hizi ni miongoni mwa mila kuu ya kidini ya Waislamu wa Yemen kwa karne nyingi na katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya watu wenye misimamo mikali wamepinga kufanyika sherehe hizo wakidai kuwa eti ni bidaa.

Hata hivyo, wanazuoni wa Kiislamu nchini Yemen na nchi nyingine za Kiislamu wameidhinisha sherehe hizo, wakisisitiza umuhimu wa kuheshimiwa hadhi ya Mtume Muhamamd (SAW) ambaye ni mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu.

Maafisa wa harakati ya Ansaullah ya Yemen pia wamekuwa na shauku ya kufanya sherehe za Milad-un-Nabi kwa ubora kadiri inavyowezekana.

Mwaka huu, sherehe hizo zitafanyika baadaye Septemba.

Wakati huo huo, tamasha la pili la kila mwaka la Milad linaendelea katika Wilaya ya at-Tahrir mjini Sana’a.

Jumuiya ya kutoa misaada ya mafundisho ya Qur’ain na sayansi imeandaa tamasha hilo litakaloendelea hadi tarehe 10 Septemba.

Mwaka huu, pia inaangazia shughuli zinazolenga kutangaza mshikamano na watu wa Palestina huku kukiwa na vita vinavyoendelea vya mauaji ya halaiki vilivyoanzishwa na utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.

/3489811

Habari zinazohusiana
captcha